Loading...

Lowassa atiwa mbaroni Geita



EDWARD Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali, anaandika Charles William.
Lowassa amekamatwa alasiri ya leo baada ya kukatiza kwa mguu katika eneo stendi ya mabasi Geita, ambapo wananchi wengi walimzunguka wakimsalimia na kusababisha msongamano mkubwa wa watu, kila mtu wakitaka kumsogelea.
Hata hivyo taarifa zaidi kutoka mkoani Geita zimeeleza kwamba, mbali na Lowassa kukamatwa lakini pia baadhi ya waandishi wa habari walipigwa na kukamatwa na askari waliofika eneo la tukio kumkamata Lowassa.

“Askari walifika wakiwa katika magari matatu huku wakiwa wamejihami kwa silaha za moto, wamewapiga waandishi wa habari na kumkamata Lowassa ambapo wamempeleka Kituo Kikuu cha Polisi Geita,” kimeeleza chanzo chetu.
Khamis Mgeja, mmoja kati ya watu waliokuwa wameambatana na Lowassa katika msafara huo amesema, Lowassa alikuwa akielekea sokoni kununua matunda na kwamba wanashangaa kwanini Polisi wamemkamata.
“Alikuwa anapita sokoni kununua matunda, watu wakajazana kumsalimia na yeye kama mtu muungwana akawa akisalimiana nao, polisi wakafika kumkamata na wamempeleka kituo kikuu cha polisi,” amesema kwa simu Mgeja alipozungumza na MwanaHALISI Online.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hili zitakujia kwa kadri tutakavyokuwa tukipokea…

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright VARWAY | Designed By VUNJAMBAVU
Back To Top